Cornel Mtavangu
TIES EditorialTanzania Integrated Engineering Solution (TIES) imekamilisha Mafunzo ya Waendeshaji Mitambo yenye mada isemayo “Misingi ya Usindikaji wa Dhahabu na Mbinu Sahihi za Uchunguzi wa Sampuli (Basics of Gold Processing and Proper Sampling Practices)”, iliyoandaliwa kwa niaba ya Stamigold Company Limited. Mafunzo haya yaliyodumu kwa siku saba kwa awamu mbili za washiriki tofauti kati ya tarehe 8 mpaka 15 April 2026 na tarehe 20 mpaka 28 April 2026, yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa huku ikihusisha washiriki 18, yakionyesha hatua muhimu katika juhudi za kuimarisha ujuzi wa kiufundi kwa waendeshaji mitambo nchini Tanzania.
Kuhusu Mafunzo
Programu hii iliandaliwa mahsusi kwa waendeshaji mitambo wa Stamigold Company Limited, ikiwa na lengo la kuwapatia ujuzi wa msingi na wa vitendo katika eneo la usindikaji wa dhahabu (Gold Processing). Washiriki walipata mafunzo kuhusu mchakato wa uchimbaji na usindikaji wa dhahabu (Gold Extraction and Processing), pamoja na taratibu sahihi za uchunguzi wa sampuli (Sampling Procedures) zinazochangia ubora wa uzalishaji pamoja na kuongeza uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali za kiutendaji (Operational Challenges).
Mada Zilizofundishwa (Training Modules)
Katika kipindi cha siku saba, washiriki walipitia mada muhimu zifuatazo:
- Usindikaji wa Dhahabu (Introduction to Gold Processing) — asili ya madini (Ore Characteristics), mbinu za uchimbaji (Mining Methods)
- Dhana za Msingi za Usindikaji wa Madini (Fundamentals of Mineral Processing) —Crushing, usagaji (Grinding), uchakataji wa kemikali (Chemical Processing), unyonyaji wa kaboni (Carbon Adsorption - CIL/CIP) na uchimbaji wa umeme (Electrowinning)
- Mfumo wa Uendeshaji wa Mitambo (Process Plant Operations) — mpangilio wa mchakato (Process Flow), kazi za vifaa (Equipment Functions) na sehemu mbalimbali za mtambo (Plant Sections)
- Vigezo vya Mchakato na Udhibiti (Process Parameters and Control) — pH, msongamano wa tope (Slurry Density), cyanide (Cyanide Levels) na oksijeni iliyoyeyushwa (Dissolved Oxygen)
- Taratibu za Uchunguzi wa Sampuli (Sampling Procedures and Protocols) — maeneo ya sampuli (Sampling Points), ukusanyaji (Sample Collection), uwekaji lebo (Labeling) na uhifadhi wa kumbukumbu (Data Recording)
- Usalama na Utatuzi wa Matatizo (Safety and Troubleshooting) — matumizi ya vifaa vya kujikinga (Personal Protective Equipment - PPE), ushughulikiaji wa kemikali (Chemical Handling) na usimamizi wa mazingira (Environmental Management)
Matokeo na Mafanikio (Outcomes and Achievements)
Mwisho wa programu, washiriki wote walitunukiwa vyeti vya kuhitimu kutoka TIES, vinavyothibitisha mafanikio yao ya kukamilisha mafunzo. Mafunzo haya yanatarajiwa kuchangia moja kwa moja katika:
- Kuongeza ufanisi (Operational Efficiency) na usalama (Safety Performance) wa uendeshaji wa mitambo ya Stamigold
- Kupunguza makosa ya kiufundi (Technical Errors) na hatari za kiusalama (Safety Risks) kazini
- Kuboresha ubora wa sampuli (Sample Quality) na usahihi wa takwimu za uzalishaji (Production Data Accuracy)
TIES inaendelea kuwa katika mstali wa mbele katika kutoa huduma za mafunzo ya hali ya juu (Professional Training Services) zinazokidhi mahitaji ya sekta ya madini nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini. Ushirikiano huu na Stamigold Company Limited ni uthibitisho wa dhamira ya pamoja ya kukuza ujuzi wa kitaaluma (Professional Capacity Building) na kuimarisha sekta ya madini kupitia wataalamu wa ndani (Local Expertise Development).
Tanzania Integrated Engineering Solution (TIES)
www.ties.co.tz
info@ties.co.tz
+255 653 405 687 | +255 753 649 039
Dar es Salaam, Tanzania


